Azam FC leo imeanza vema ligi kuu baada ya kuichapa Tanzania Prisons mabao 2-1.

 

Ni Muivory Coast Kipre Tchetche ndiye aliiandikia Azam FC bao la kwanza katika dakika ya 39 baada ya kupiga shuti kali lililomwacha kipa wa Prisons Mohamed Yusuph akigaagaa.

 

Prisons walirudi kipindi cha pili na nguvu wakapata bao la kusawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Jeremiah Juma aliyepiga shuti kali.

 

Azam FC iliyotumia mfumo wake wa kawaida wa 3-5-2 iliongeza bao la pili na la ushindi kupitia kwa kinda Farid Mussa ambaye alipata pasi kutoka kwa Salum Aboubakary ‘Sure Boy’ katikati ya uwanja ambapo aliukokota hadi golini na kufunga.

 

Hata hivyo, Azam FC ingeshinda mabao zaidi ya manne kwani straika wao Mkenya Allan Wanga alipoteza nafasi nyingi za mabao dakika ya 25 baada ya kichwa chake kugonga mwamba na kudakwa na kichwa na dakika ya 45 kichwa chake kilitoka nje.

 

Kocha mkuu wa Azam Stewart Hall amesema,. amefurahia ushindi walioupata licha ya kuwa walipoteza nafasi nyingi za mabao.

 

Azam FC

Aishi Salum 2.Aggrey Morris 3.David Mwantika. 4Serge Wawa. 5 Erasto Nyoni, 6 Mugiraneza Jean Baptiste/ Ramadhani Singano ‘Messi’ dk 78. 7 sALUM aboubakary ‘Sure Boy’, 8 Mudathir Yahya/ Himid Mao dk 60, 9 Allan Wanga / Ame Ally dk 68, 11 Farid Muussa.