Hakuna kumtuma mtoto dukani ndivyo unavyoweza kuutabiri ushindani wa mtanange wa kesho kati ya Azam FC na Tanzania Prisons mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex.

 

Hii inatokana na matokeo yaliyopita katika miaka miwili mfululizo ambapo Tanzania Prisons imeibuka kuwa moja ya timu zinazopata matokeo ya kustaajabisha Chamazi.

 

Prisons kwa misimu wiwili mfululizo imekataa kufungwa na Azam FC hali iliyoamsha mihemuko ya wachezaji wa pande zote mbili. Kesho jioni timu hizi zenye uzoefu na ligi kuu zitakwaana kwenye mechi ya ufunguzi VPL.

 

Akizingumza na tovuti hii, mtendaji mkuu wa Azam FC ndugu Saad Kawembe alisema taratibu zote za maandalizi ikiwemo kupata vibali vya wachezaji wote wa ndani nan je ya nchi vimekamilika kwa 100%. Kilichobaki ni kuingiz uwanjani.

 

Nahodha wa zamani wa Azam FC Aggrey Morris akiwa na nahodha msaidizi Salum Abubakar Sure-boy alisema, tupo tayari kwa mpambano. Tumejiandaa vizuri na inshallah tutashinda kesho.

 

Kocha mkuu wa Azam FC Stewart Hall alisema kwenye hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa maalum kuwapongeza wachezaji kwa mafanikio ya ushindi wa Kagame Cup na kuwatakia kila la kheri kwenye mtanange wa VPL msimu unaoanza “maandalizi yetu yalichukua muda mrefu na mechi nyingi, sasa ni wakati wa kuonesha kwa vitendo uwanjani. Uongozi umetupa kila tulichohitaji. Sasa ni wakati wetu kulipa kwa kucheza kwa bidii na kushinda kila mechi alimalizia Stewart”

 

Azam FC itafungua dimba kwa kucheza na Tanzania Prisons kesho Jumamosi tarehe 12/09/2015 kisha itasafiri kwenye Shinyanga kukwaana na Stand United na Mwadui FC Jumatano na Jumapili ijayo.