Beki mpya wa Azam FC, Racine Diof ameonyesha kwamba kwake ni kazi tu, baada ya kufanya mazoezi mara mbili.

 

Diof alifanya chini ya kocha wake Stewart na baadaye baada ya wenzake kuondoka, aliungana na vijana wawili wa timu B na kwenda gym akafanya mazoezi yake binafsi. Hapo alifanya ya viungo tofauti kwa kutumia mashine na bila mashine.

 

Alisema, anapenda kufanya mazoezi mengi kutokana na kile anachokiamini kuwa, ndiyo siri ya mafanikio. Diof ni beki mpya wa kimataifa wa Azam FC ambaye amesajiliwa hivi karibuni