Timu ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo itakuwa na kibarua kigumu cha kukwaana na Super Eagles katika mchezo wa Kundi G, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Saa 10: 30 jioni.
Mara ya mwisho Tanzania kukutana na Nigeria ilikuwa Septemba 11, mwaka 2002 katika mechi ya kirafiki na Super Eagles ilishinda 2-0. 

Mshauri wa Ufundi wa Taifa Stars, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ ambaye alicheza mechi dhidi ya Nigeria kwenye Michezo ya Afrika mwaka 1973. Leo atakuwa kwenye benchi la taifa stars linaloongozwa na wazawa Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco.

Kikosi cha Taifa Stars kwa sasa kianaoneka kutoa matumaini hasa kutokana na kujumuisha nyota wote waliopo Tanzania kwa sasa. Mbwana Ally Samata, Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngassa, Simon Msuva, Farid Mussa na John Bocco wanatarajia kuongoza mashambulizi ya Taifa Stars  huku Frank Domayo, Himid Mao, Mudathir Yahya, Said Ndemla, Salum Telela na Deus Kaseke wakitarajiwa kucheza sehemu ya kiungo.

Mmoja kati ya magolikipa Ally Mustafa, Said Mohamed, ataanza akilindwa na walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, Kelvin Yondani, Hassan Isihaka na nahodha Nadri Haroub “Cannavaro”.

Azam FC inaitakia kila la kheri