Azam FC kwa mara nyingine tena imepoteza ngao ya jamii baada kulazimishwa suluhu ya bila kufungana Yanga ambao baadaye waliwatoa kwa njia ya mikwaju ya penalti 8-7 wakachukua ubingwa wa Ngao ya Jamii.

 

Katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ulikuwa wa ushindani mkubwa kila timu ilionyesha ubabe kwa mwenzake wakishambuliana  kwa zamu lakini hadi dakika zote 90 zinamalizika, hakuna aliyeona lango la mwenzake.

 

Na kutokana na kanuni za mchezo huo, mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro aliamuru zipigwe penati ambapo Azam FC walipata penalti kupitia kwa Muivory Coast Kipre Tchetche, John Bocco ‘Adebayor’, Himid Mao, Aggrey Morris, Mnyarwanda Mugiraneza Jean Baptiste, Erasto Nyoni na Shomari Kapombe, lakini Muivory Coast Serge Wawa na Ame Ally walikosa.

 

Kwa upande wa Yanga waliopata ni Mnyarwanda Haruna Niyonzima ‘Fabregas’, Deus Kaseke, Mrundi Tambwe Amissi, Mbrazil Andrey Coutinho, Geofrey Mwashiuya, Thaban Kamusoko, Mnyarwanda Mbuyu Twite na Kelvin Yondani ‘Vidic’ huku nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ya kwake iliokolewa na kipa wa Azam Aishi Manula.

 

 

 

Dakika 90

 

Ndani ya mchezo huo dakika ya 7, Kipre alikosa bao la wazi baada ya shuti lake kuchezwa na Bartez, hata hivyo dakika 27 Manula alifanya kazi ya ziada mpira wa kichwa uliokuwa umepigwa na Ngoma.

 

 

 

Vikosi

 

Azam

 

 1. Aishi Manula, 2. Shomari Kapombe, 3 Erasto Nyoni, 4.Aggrey Morris, 5. Serge Wawa, 6. Himid Mao, 7. Frank Domayo/Ame Ally,  8. Mudathir Yahya/ Mugirameza, 9. Bocco, 10. Tchetche, 11. Farid Mussa.

 

 

 

Yanga

 

1. Ally Mustapha ‘Bartez’, 2. Mbuyu Twite, 3.Haji Ngwali, 4. Cannavaro, 5. Yondani, 6. Said Nakapu/Niyonzima, 7. Simon Msuva/Coitunho, 8.Thaman Kamusoko, 9. Tambwe, 10. Donaldo Ngoma/Kaseke, 11. Mwashiuya.