Kikosi cha Azam FC chini ya Stewart John Hall kimerejea jana toka visiwani Zanzibar kilikoweka kambi ya wiki moja kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Jumamosi tarehe 22/08/2015

 

Azam FC ambao ni mabingwa wa CECAFA Kagame Cup, wamepania kuhakikisha wanatwaa Ngao hiyo ambayo mara tatu wameipoteza dhidi ya Simba na Yanga.

 

Kikosi cha Azam FC kimeimarika sana baada ya kurejea Stewart Hall ambaye amejenga ngome imara ya ulinzi huku akibadilisha mfumo wa uchezaji toka 4-3-3 uliozoeleka na sasa Azam FC inacheza mfumo wa 3-5-2

 

Azam FC ambayo kwenye mashindano ya CECAFA ya Kagame Cup iliwakosa nyota wake kadhaa kama Allan Wanga na Ramadhan Singano Messi, imejipanga kuhakikisha inashinda kila kikombe kilicho mbele yake.