Rais Dr Jakaya kikwete ambaye ni mpenzi wa michezo na burudani alipotembelewa na wachezaji wa Azam FC ikulu jana alisema, Baada ya kusikia Azam FC imeshinda alifurahi na kuongeza kwamba ushindi huo umepunguza ukame wa vikombe vya mashindano ya kimataifa kwa klabu za hapa nchini.
“Hongereni sana, maana mmeshinda, ingekuwa wengine wangeanza kutoa sababu ambazo si za kimpira, mara marefa, mchezaji mmoja…

Nawatakia kila la kheri mshinde kikombe hiki mara tatu mfululizo hadi kiwe chenu moja kwa moja. Pia muelekeze nguvu Afrika sasa kwani tunataka ubingwa wa Afrika alisema Rais Kikwete.