Kipa wa Azam FC, Aishi Manula amesema, kikosi chao kimefanya vizuri hadi kuchukua kombe kwa sababu walicheza kwa malengo na ushirikiano wa hali ya juu wakikubaliana mapema “atakayekosea atakemewa”.

 

Manula ambaye alidaka mechi tano kati ya sita walizocheza Azam FC kuanzia hatua ya makundi hadi fainali na mwenzake Mwadini Ally alidaka moja tu alicheza kwa ustadi wa hali ya juu kiasi cha kutangazwa kuwa mlinda lango bora wa mashindano na waandaaji..

 

Amesema: “Hii ni historia kwetu hivyo wachezaji tukacheza kwa kujituma na kushirikiana lakini kila mmoja akitambua majukumu yake na tulikubaliana, atakayekwenda kinyume hataachwa lazima akumbushwe.”

 

“Pia nidhamu tulicheza kwa nidhamu kwa kufuata maelekezo ya kocha wetu na kujitambua, lengo letu lilikuwa moja ndiyo maana ikawa rahisi kwetu.”