Kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema, ana kila sababu ya kushinda mechi ya fainali itakayochezwa leo Jumapili dhidi ya Gor Mahia ya Kenya Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

 

Azam FC ambayo itaendelea kumkosa kiungo wake Salum Aboubakary ‘Sure Boy’ mwenye maumivu ya enka lakini wachezaji wengine wote wako fiti.

 

Imefanya maandalizi ya kutosha ambapo Stewart amesisitiza fomesheni yake 3-5-2 itatosha kabisa kuwamaliza wajaluo, timu inashoshabikiwa na nahodha wa zamani wa Azam FC Ibrahim Shikanda. amewaita mashabiki wapenda soka, wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuona burudani safi.

 

“Tunacheza na Gor Mahia, ni timu nzuri, wana nguvu na wanashirikian, lakini kwa upande wetu nasi tumejiandaa kushinda,”alisema Stewart.