Ikitumia mfumo wa 3-5-2 Azam FC imekuwa na ngome imara ya ulinzi na hadi inaingia mechi ya fainali leo hii dhidi ya Gor Mahia, haijaruhusu hata bao moja la kufungwa kikosini mwao.

 

Ukuta huo, unaongozwa na Waziri wa Ulinzi, Muivory Coast Serge Wawa, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Said Morrad na Abdallah Kheri ambao wamekuwa wakipangwa kwa nyakati tofauti, wamekuwa tishio mbele ya washambuliaji wabishi.

 

Kocha wao mkuu Stewart Hall amesema, nidhamu ndiyo imekuwa chchu ya mafanikio yao lakini pamoja uimara wa mabeki hao, suala la ulinzi limekuwa jukumu la wachezaji wote 11.

 

“Timu imekuwa ikicheza kwa ushirikiano na uimara wa Azam kwenye ulinzi ni suala la wachezaji wote 11 licha ya kuwa, safu ya ulinzi kufanya kazi yao kwa ufasaha,’alisema Stewart.

 

Mtokeo ya Azam hatua ya makundi ilicheza na KCCA 1-0, Malakia 2-0, Adama City 5-0. Hatua ya robo fainali, iliifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti 5-3 baada ya kumaliza kwa suluhu 0-0 na nusu fainali, imeichapa KCCA bao 1-0.