Kocha mkuu wa KCCA ya Uganda, Sam Ssimbwa ameshindwa kuvumilia na kutamka, Azam FC ni hatari.

 

Ssimbwa ametamka hayo baada ya kupokea kichapo mara mbili kutoka kwa Azam katika hatua ya makundi alipigwa 1-0 mfungaji John Bocco  na mechi ya nusu fainali, alipochapwa 1-0 alifunga Farid Mussa.

 

Hata Hivyo, Ssimbwa hakutaka kutupa shiringi yake moja kwa moja kwa kuwa Azam FC inaweza kuchuku ubingwa na kusema: “Wacha tusubiri tuone.”

 

Lakini akasifu safu ya Azam FC ya ulinzi ambayo haijaruhusu hata bao moja mpaka sasa, ni ngumu kuingilika na itawapa ugumu Gor Mahia.