AZAM FC imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya CECAFA Kagame Cupbaada ya ushindi wa penalty 5-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, shujaa wa Azam FC alikuwa ni kipa Aishi Salum Manula aliyepangua penalti ya beki mpya wa kushoto wa Yanga SC, Mwinyi Hajji Mngwali.

Wachezaji Kipre Herman Tchetche, Serge Wawa Pascal wote raia wa Ivory Coast, John Bocco, Himid Mao na Aggrey Morris walifunga penati zao, wakati za Yanga SC zilifungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela na Godfrey Mwashiuya.  

katika mtanange wa dakika tisini Azam FC iliutawala mchezo hasa kipindi cha kwanza na kukosa magoli mengi kupitia kwa John Bocco, Kipre Tchetche na Shomari Kapombe

 

 

Azam FC sasa itamenyana na KCCA ya Uganda katika Nusu ya pili Ijumaa, baada ya Khartoum N na Gor Mahia kupambana katika Nusu Fainali ya kwanza.

Utamu ni kwamba, Nusu Fainali zote zitakuwa marudio ya mechi za makundi, kwanza Azam FC iliifunga 1-0 KCCA katika mechi ya Kundi C na Khartoum N ilitoka sare ya 1-1 na Gor Mahia katika mchezo wa Kundi A.

Farid Mussa kwa mara nyingine alikuwa nyota wa mchezo wa leo

Kikosi cha Azam FC kilikuwa: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Agrey Morris, Abdallah Kheri/Said Mourad dk46, Paschal Wawa, Jean Mugiraneza, Himid Mao, Frank Domayo/Ame Ally dk46, Farid Mussa, John Bocco na Kipre Tchetche. 
Yanga SC: Ally Mustafa ‘Barthez’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul/Joseph Zuttah dk69, Godfrey Mwashiuya, Donald Ngoma, Kevin Yondani, Mbuyu Twite, Deus Kaseke/Salum Telela dk61, Amisi Tambwe, Haruna Niyonzima/Malimi Busungu dk80 na Hajji Mwinyi.