Azam FC imeweka historia kwenye mashindano ya Kombe la Kagame yanayoendelea jijini Dar es Salaam katika hatua ya makundi baada ya kumaliza mechi zote tatu bila kuruhusu bao hata moja la kufungwa na wachezaji wao, walizoa zawadi zote za uchezaji bora ‘Man of the Match’.

 

Azam ilipangwa kundi C pamoja na timu za Malakia, Adama City na KCCA

 

Katika mechi ya kwanza waliyocheza na KCCA, Azam FC kupitia kwa kiungo wake, Salum Aboubakary ‘Sure Boy’ alijinyakulia zawadi ya king’amuzi cha DSTV kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo na matokeo Azam FC ilishinda bao 1-0. Goli likifungwa na nahodha wake John Bocco.

 

Mechi ya pili waliyoshinda mabao 2-0 dhidi ya Malakia,  beki wao wa kati,  Muivory Coast Serge Wawa Pascal alijinyakulia zawadi ya aina hiyo huku Bocco tena na Kipre Tchetche wakiibuka wafungaji bora.

 

Mechi  ya tatu ya kukamilisha hatua hiyo ya makundi dhidi ya Malakia wakashinda 5-0, winga wao chipukizi, Farid Mussa alipata zawadi ya hiyo huku Kipre Tcheche akifunga magoli mawili, Farid Mussa akifunga moja, mengine yakifungwa na Mudathir Yahya na Aggrey Morris kwa njia ya penati