Ikicheza soka safi la hali ya juu na kuelewana muda wote wa dakika 90, Azam FC leo imeigalagaza vibaya Adama City FC jumla ya mabao 5-0 na kujihakikishia uongozi wa kundi kwa “style” mbali na kutinga robo fainali huku huku nyavu zake zikiwa hazijaguswa.

 

Wiinga kinda mwenye kipaji cha hali ya juu Farid “Maliki” Mussa  Shah kiibuka mchezaji bora wa mechi na kukomba zawazi toka wa wadhamini DSTV.

 

Azam FC waliandika bao la kwanza kupitia kwa Kipre Tchetche dakika ya saba akimalizia  pasi kutoka kwa Amme Ally Zungu.

 

Kipre aliipatia tena bao la pili dakika 19, alikuwa kwenye engo kilipo kibendela nje kabisa ya 18, akamwangalia mlinda lango wa Adama City, Yacob Fiseha alivyokaa na kupiga mpira kiufundi uliokwenda moja moja golini.

 

Azam FC ilipachika tena bao la tatu dakika dakika ya 32 kupitia kwa Farid Mussa.

 

Azam ilianza kipindi cha pili kwa kasi na kupata bao la nne dakika ya 49 lililofungwa na Mudathir Yahya kwa kichwa kabla ya Aggrey Morris kufunga kalamu ya mabao alipopachika la tano kwa njia ya penalti dakika ya 69.

 

Penalti hiyo ilipatikana baada ya Mogesi Tadese  wa Adama City kuokoa kwa mkono, shuti la Mudathir na akatolewa kwa kadi nyekundu.

 

Pia beki mwingine wa Adama Eshetu Menna alitolewa nje kwa kadi nyekundu.