Ikitumia mfumo wa 3-5-2 Azam FC leo imeichapa KCCA ya Uganda bao 1-0 goli lililofungwa na straika na nahodha John Bocco ‘Adebayor’

Bocco aliiandikia bao hilo pekee lililowapa ushindi na pointi tatu dakika 11 kutokana na pasi ya Salum Aboubakary ‘Sure Boy. Kabla ya kufunga Bocco alimfinya beki wa KCCA na kufunga kwa ufundi.

Azam iliyokuwa inacheza soka ya kuvutia kwa fomesheni hiyo ya 3-5-2 ambapo nyuma aliwatumia mabeki wa kati watatu Serge Wawa, Aggrey Morris na Said Morrad na kiungo kati akacheza Sure Boy, Himid Mao na Frank Domayo ikawafanya wang’are zaidi.

 

Ilifanya mabadiliko dakika ya 46 kwa kumtoa Mrundi Didier Kavumbagu na Muivory Coast Kipre Tchetche kuchukua nafasi, dakika 65 Frank Domayo alitoka akaingia Mnyarwanda Mugiraneza Jean Baptiste, dakika 82 alitoka Sure Boy akaingia Mudathir Yahya.

Kocha mkuu wa Azam Stewart Hall alisema, anashukuru kupata ushindi huo, vijana wake walicheza kwa kufuata ,maelekezo ndiyo maana walishinda. Pia fomesheni waliyobadili ni moja ya sababu ya ushindi huo.

 

Azam

Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Serge Wawa, Aggrey Morris, Said Morrad, Himid Mao, Salum Aboubakary ‘Sure Boy, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, John Bocco.

 

KCCA

Ochan Benjamin, Masiko Tom, Kavuma Habib, Mpuga Martin, Wasswa Hassan, Senkumba Hakim, Okot Denis, Nsibabambi Derrick, Mutyaba Muzamir, Ochaya Joseph Birung Michael.