Straika Mrundi wa Azam FC, Didier Kavumbagu amekubali ufundi anaoupata kutoka kwa kocha wake, Muingereza Stewart Hall na akatamba kwamba huyu kocha anajua sana.

Kavumbagu amefundishwa na makocha tofauti akiwemo Mcameroon Joseph Omog ambaye alimalizana na Azam FC  baada ya kushindwa kufikia mafanikio ya matakwa ya mkataba wake alisema: “Nimekaa na kocha Stewart kwa muda mchache lakini namwelewa sana, ana mazoezi mazuri na ufundi wake uko juu sana. Naweza kusema ni bonge la kocha.”

“Nimefundishwa na makocha tofauti lakini huyu hata anavyofundisha unaona kuna vitu vizuri,:alisema Kavumagu.

Kavumbagu anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Azam FC kitakachoshiriki CECAFA Kagame Cup mashindano yanayoanza kesho.