Kiraka wa Azam FC Shomari Kapombe, amesema timu yao iko tayari kwa Kagame na wana kila sababu ya kuchukua Kombe hilo msimu huu na kutengeneza historia mpya ya klabu.

Kapombe amesema, ana jeuri ya kusema hivyo kutokana na aina ya wachezaji walionao kikosini kila idara kuanzia ulinzi hadi ushambuliaji imetimia.

“Kwa kawaida, mashindano yote ni magumu ndiyo maana yakaitwa mashindano, lakini safari hii nina kila sababu ya kusema tuko tayari kwa mapambano na hii ni kutokana na namna timu ilivyo vizuri kuanzia nyuma kwenye ulinzi hadi ushambuliaji,”alisema Kapombe.

Hata hivyo, Kapombe alianza mazoezi jana na alifanya kwa kasi, licha ya kuwa ametoka kuugua malaria yaliyomwekaa nje ya uwanja kwa siku kadhaa.