Kikosi kamili cha Azam FC kesho kitaingia kambini tayari kujiwinda rasmi na michuano ya Kombe la Kagame, wachezaji hao, wataambatana na benchi lao la ufundi kwenda kula sikuu ya Idd kwenye kasir la familia ya Bakhresa Kigamboni.

Kocha mkuu wa kikosi hicho, Stewart Hall anatarajia kuchagua wachezaji 20 watakaocheza michuano hiyo kulingana na mujibu wa kanuni za mashindano hayo ya Kagame , lakini amesisitiza amejiandaa vizuri na kikosi kipo sawa kabisa.

Kambi hiyo itakuwa kwenye hosteli zao zilizopo Chamazi, Mbagala.