Winga wa kimataifa wa Tanzania Ramadhan Singano Messi leo amejiunga na klabu ya Azam FC baada ya kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF kumtangaza kuwa mchezaji huru juzi.

Azam FC inamkaribisha Singano kwenye kikosi chake tukitarajia kupata huduma yake itakayoisaidia Azam FC kupiga hatua katika harakati za kujenga kikosi bora nchini