Ikijaribu mfumo mpya wa 3-5-2 Azam FC imefanikiwa kuifunga JKT Ruvu bao 1-0 Shukrani kwa goli la dakika ya 89 la Mshambulizi aliyeingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Dedier Kavumbagu Muaivory Coast Kipre Herman Tchetche

 

Mechi hii ya kusisimua ilichezwa kwenye uwanja wa Chamazi complex, JKT Ruvu ilijitutumua na kucheza soka safi lakini habati ya kupata goli haikuwa upande wao. Kipre alifunga goli hilo la Azam FC dakika nne tuubaada ya kuingia akiunganisha krosi ya kiungo aliyecheza vizuri sana Salum Abubakar.

Ingawa mechi ya leo ilikuwa na lengo la kumjaribu golikipa mpya toka  Ivory Coast, Vincent Atchouailou de Paul Angban aliyewahi kudakia timu ya vijana ya klabu bingwa England, Chelsea FC lakini benchi la ufundi lililazimika kumuacha kumpa muda wa kujiandaa kutokana na kutoka likizo na kuhitaji mazoezi ya kusaka wepesi kabla hajapewa muda wa majaribio.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa;

Golikipa; Aishi Manula,

 

Walinzi watatu walianza David Mwantika/Said Mourad, Aggrey Morris, Abdallah Kheri/Serge Wawa,

 

Walinzi wa Pembeni walicheza; Erasto Nyoni, Brian Majwega/Gardiel Michael.

 

Viungo walicheza; Himid Mao, Bryson Raphael/Kipre Bolou, Salum Abubakar ‘Sure Boy’,

Washambuliaji walicheza; Kevin Friday/Farid Mussa Malik na Didier Kavumbangu/Kipre Tchetche.

JKT Ruvu; Tony Kavishe, Napho Zubeiry, Jaffar Kisoky, Kisimba Luambano, Martin Kazila/Bhinda Abdallah, Hamisi Shengo, Ismail Aziz, Mateo Saad/Yohana Misanya, Alex Abel, Saad Kipanga na Emmanuel Pius/Daud John.