Tembo toka Afrika Magharibi straika, Kipre Tchetche na difenda Serge Wawa Pascal wameungana na  Brien Majwega raia wa Uganda, Kipre Bolou na Mrundi Didier Kavumbagu na kukamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni wanaohudhuria mazoezi ya ya Azam FC kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza katikati ya mwezi huu.

Tchetche na Wawa wamewasili wikiendi hii, Majwega alikuwa anasumbuliwa na malaria na homa ya matumbo sasa amepona kabisa, wote kwa pamoja, wataungana na wachezaji wenzao katika mazoezi hayo ya Jumatatu.

 

Kocha wa Azam Stewart Hall alisema: “Jumatatu natarajia kuwa na wachezaji wangu wote na watakaokosekana ni wale tu waliokuwa na Taifa Stars.”

 

“Tchetche, Wawa wameshawasili, Majegwa aliyekuwa mgonjwa Erasto Nyoni aliyekuwa na Stars wote wataanza mazoezi na wenzao.” pia wapo baadhi waliokuja kusaka nafasi ya kusajiliwa. Jumanne Azam FC itacheza na JKT Ruvu katika mchezo wa kirafiki