Azam FC inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na  JKT Ruvu  kwenye Uwanja wa Azam Complex kesho Jumanne jioni, mchezo ambao kocha Stewart Hall atautumia kuwapima wachezaji wake akiwemo mlinda Mlango Muivory Coast, Vincent Atchouailou de Paul Angban.

 

Vincent ametua Dar es Salaam wikiendi iliyopita na Jumanne atacheza mchezo huo wa kwanza kwenye kikosi cha Azam na JKT inayonolewa na kocha, Fred Minziro.

 

Stewart alisema: “Tunaendelea vizuri na mazoezi na Jumanne tutacheza mechi ya kirafiki na JKT kwa ajili ya kujipima. Katika mchezo huo, natarajia kumtumia kipa Muivory Coast aliyewasili wikiendi hii kwa majaribio.”

 

Huo ni mchezo wa pili wa Azam wa kirafiki baada ya ule wa kwanza wa wiki iliyopita, waliocheza na France Rangers wakashinda 4-2.