Wakati mazoezi ya timu ya soka ya Azam FC yakiwa yameanza huku timu ikiwakosa nyota wake wengi kutokana na kuwa na majukumu kwenye timu za taifa kikosi cha under 20 kimenogesha mazoezi hayo.

Vijana hao wa kikosi cha vijana wamefanya mazoezi na kaka zao ya kujiandaa na msimu mpya na mashindano ya Kagame Cup. benchi jipya la Azam FC limefurahia vipaji ilivyovikuta.

Azam FC chini ya Stewart Hall imekuwa ikijifua kujiandaa na mashindano ya Kagame Cup yatakayofanyika nchini mwezi ujao