Uongozi wa Azam FC upo katika hatua za mwisho kumsajili mlinda lango wa Jeunesse ya Ivory Coast Vincent Atchouailou de Paul Angban.

Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili wiki ijayo akiambatana na Kipre Tchetche, Kipre Bolou, na Serge Wawa Pascal kwa ajili ya kusaini Mkataba wa kujiunga na Azam FC. 

Mlinda mlango huyo aliyezaliwa Februari 2, mwaka 1985 mjini Anyama, pia amewahi kufanya majaribio na kucheza kwenye timu ya wachezaji wa akiba wa Chelsea ya England.

Kipa huyo aliyeibukia katika klabu ya vijana ya Rio Sport d’Anyama amwewahi chezea klabu ya Sawe Sports msimu wa 2006/2007, ASEC Mimosas
2007/2009 kabla ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Daniel Yeboah. 

Amewahi kudakia timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Ivory Coast katika michuano ya Afrika nchini Benin mwaka 2005 na aliiwakilisha pia nchi yake katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2008.