Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeanza vibaya mechi za Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 baada ya kufungwa mabao 3-0 na Misri usiku wa jana mjini Alexandria.
Mabao yote ya Misri yalipatikana kipindi cha pili, wafungaji wakiwa ni Rami Rabia dakika ya 61, Basem Morsi dakika ya 65 na Mohamed Salah dakika ya 70.