Mkurugenzi wa Fedha na utawala wa Azam FC toka nchini Uingereza pamoja na wasaidizi wa benchi la ufundi kuwasili ijumaa hii tayari kuanza kazi Azam FC

 

Kufuatia mabadliko makubwa ya watendaji na mfumo wake wa uongozi, benchi la ufundi la Azam FC sasa litakuwa chini ya Stewart Hall ambaye yupo jijini Dar es Salaam akisubiri kuwapokea wasaidizi wake ijumaa hii.

 

 

Watakaowasili ni pamoja na muingereza mwenye asili ya Uganda Eli Eribankya ambaye atakuwa Meneja utawala na fedha. Eribankya atasaidiwa na mwanandinga wa zamani wa Azam FC mtanzania Luckson Kakolaki.

Stewart John Hall ambaye anarejea kwa mara ya tatu kuongoza benchi la ufundi la Azam FC. atasaidiwa na Mganda George Best Nsimbe, huku Mark Philips kutoka uingereza akiajiriwa kuwa kocha wa magolikipa. Hawa wote watawasili ijumaa hii.

 

Wengine watakaowasili ni Mark Philips atakayekuwa kocha wa magolikipa. Mtaalamu wa tiba ya viungo na lishe “Team Physiotherapist and Nutritionist” Bwana George Adrian Dobre kutoka Romania na Mario Marian Anton Marinica kutoka Romania atakayeongoza benchi la ufundi la timu ya vijana.

 

Azam FC itaanza mazoezi kujiandaa na Kagame Cup Jumanne ijayo