Himid Mao Mkamy na Aishi Salum Manula wamepigiwa chapuo na mashabiki wengi wa Azam FC mtandaoni kuwa wachezaji bora wa klabu msimu wa 2014/15.

 

Mara baada ya ligi kuu kuisha, katika majadiliano kwa njia ya WhatsApp mashabiki  wengi walioungana na kuunda kundi linalojulikana kwa jina la Azam Die hard fans walimpigia kura Himid kuwa anafaa kupewa tuzo ya Mchezaji Bora wa klabu.

 

Mtandao huu pia ulifanya majadiliano na mashabiki toka kikundi cha Maji Matitu ambao pia wengi walimpigia kura Himid Mao.

Mwezi mmoja ukiwa umepita tangia ligi kuu imalizike Azam FC ikishika nafasi ya pili Mtandao huu uliwauliza tena swali la nani mchezaji bora wa msimu mashabiki wa Azam FC walio kwenye kundi lililoungana kwa njia ya mtandao wa WhatsApp la Azam FC Die Hard Fans. Katika majibu yao safari hii walionekana kugawanyika baadhi wakisema Aishi Salum Manula na wengine Himid Mao Mkamy.

 

Mtandao huu unawapongeza Himid Mao na Aishi Salum Manula kwa kiwango kizuri walichoonesha na kuwataka waendelee kujituma kuwa mfano wa aina ya wachezaji ambao Azam FC inawahitaji