Azam FC inatarajia kuanza mazoezi jumanne ijayo tarehe 16 kujiandaa ligi kuu msimu wa 2015/16 na mashindano ya kombe la Kagame litakalotimua vumbi jijini Dar es Salaam kuanzia July 11 mwaka huu. Kikosi cha Azam FC chini ya Kocha mwenye uzoefu na ligi ya Tanzania na klabu ya Azam FC Stewart Hall aliyerejeshwa kukinoa kikosi hicho kimedhamiria kufanya makubwa msimu huu. Azam FC ambayo imewaruhusu wachezaji wake watatu kuondoka ambao ni Amri Kiemba, Gaudence Mwaikimba na Wandwi Jackson ipo katika mawindo ya wachezaji kadhaa wa ndani na nje ya nchi ili kuimarisha kikosi chake na kukiongezea nguvu. Kinachosubiriwa ni taarifa rasmi toka TFF juu ya idadi ya wachezaji wa kigeni, hilo likishajulikana, uongozi utakaa na Benchi la ufundi kisha kuamua ni wachezaji gani toka nchi gani wanaohitajika kuongeza nguvu alisema Mtendaji Mkuu wa Azam FC Saad kawemba katika mahojiano yake na tovuti ya klabu.