MABINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC wanatarajiwa kuondoka kesho Dar es Salaam kwenda Kampala, Uganda kuweka kambi ya siku 10 kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema kwamba ziara hiyo ni maalum kwa timu kujiandaa na Ligi Kuu na kikosi kitarejea Desemba 22, mwaka huu.
Ligi Kuu iliyosimama kwa muda Novemba 9, baada ya mechi saba, inatarajiwa kuanza tena Desemba 26, mwaka huu.

Azam FC imefanya usajili wa wachezaji wawili tu katika dirisha dogo, ambao beki wa kati Serge Wawa Pascal, raia wa Ivory Coast aliyekuwa anacheza El Merreikh ya Sudan na kiungo Amri Kiemba aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka Simba SC.
Pamoja na hayo, mabingwa hao wa Tanzania Bara wamemchukua kocha Mganda, George ‘Best’ Nsimbe kuziba pengo la Muingereza, Kali Ongala aliyejiuzulu baada ya mechi sita.
Azam FC imeonyesha iko vizuri chini ya benchi jipya la ufundi, linaloongozwa na kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog baada ya jana kuwafunga vinara wa Ligi Kuu, Mtibwa Sugar mabao 3-1.