BAO pekee la Jacob Massawe dakika ya 15 limeipa ushindi wa 1-0 Ndanda FC dhidi ya mabingwa watetezi, Azam FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Huo unakuwa mchezo wa pili mfululizo, Azam kupoteza baada ya Jumamosi iliyopita kuchapwa 1-0 pia na JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Matokeo hayo, yanaifanya timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Awadh Bakhresa na familia yake ibaki na pointi zake 10, baada ya mechi sita, wakati Ndanda saa inadikisha pointi sita.
Mechi nyingine za ligi hiyo leo, Coastal Union imeilaza 1-0 Ruvu Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga bao pekee la Itubu Imbem dakika ya 54, wakati JKT Ruvu imefungwa 2-1 na Polisi Moro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. 

Leave a comment