AZAM FC imeilaza bao 1-0 Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni hii Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Shukrani kwake, beki Aggrey Morris akiyefunga bao hilo pekee dakika ya 19 kwa shuti kali la mpira wa adhabu kutoka umbali wa miya 20, kufuatia Didier Kavumbangu kuangushwa na Yohanna Morris wa Mbeya City.
Ushindi huo, unawafanya mabingwa hao wateteziAzam FC watimize pointi 10, baada ya mechi nne na kupanda kileleni kwa wastani wa mabao, baada ya Mtibwa Sugar kulazimishwa sare ya bila kufungana na Polisi mjini MorogoroMbeya City kwenye Uwanja huu, baada ya Aprili 13 mwaka huu kuichapa pia mabao 2-1 katika mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Kipa Aishi Manula leo alikuwa shujaa upande wa Azam FC kutokana na kuokoa michomo mingi ya hatari.
Kikosi cha Mbeya City kilikuwa; David Burhan, Deogratius Julius, Hassan Mwasapili, Yussuf Abdallah, Yohana Morris, Anthony Matogolo, Saad Kipanga/Peter Mwalyanzi, Steven Mazanda, Paul Nonga, Mwagane Yeya na Deus Kaseke.
Azam FC; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Mbaga, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Erasto Nyoni, Didier Kavumbangu/Gaudence Mwaikimba, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Kipre Tchetche/Mudathir Yahya

Leave a comment