Azam FC inaondoka kesho Dar es Salaam kwenda Mbeya kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa ugenini Ligi Kuu dhidi ya wenyeji Prisons Jumamosi, Uwanja wa Sokoine.
Hata hivyo, Meneja wa Azam FC, Jemedari Said Kazumari amesema kwamba beki David Mwantika na kiungo Kevin Friday hawatasafiri kwa sababu ni majeruhi. Amesema Mwantika aliumia kifundo cha mguu katika mechi na Ruvu Shooting, wakati Friday anasumbuliwa na maumivu ya misuli.
 vijana wote watakuwa nje kwa wiki moja tu. Tukirudi kutoka Mbeya, naamini watakuwa wako fiti tayari na kuungana na wenzao,”amesema.
Tayari Azam FC inawakosa Nahodha wake, John Bocco ‘Adebayor’, Frank Domayo, Joseph Kimwaga na Leonel Saint Preux, ambao wote ni majeruhi pia.
Azam FC imeanza vyema mbio za kutetea taji lake msimu huu, baada ya kushinda mechi mbili mfululizo za awali, kwanza 3-1 dhidi ya Polisi Morogoro na baadaye 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Leave a comment