AZAM FC waliochukua nafasi ya Yanga SC kwenye Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, leo wameifumua KMKM ya Zanziabr mabao 4-0 katika mchezo wa Kundi A, Uwanja wa Amahoro, Kigali.
Azam FC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao 3-0, mawili akifunga mshambuliaji wa kimataifa wa Haiti, Leonel Saint Preux na lingine Nahodha John Bocco. Adebayor.
Alianza mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Bocco au Adebayor aliyefunga bao la kwanza dakika ya kwanza tu kabla Leonel kufunga mara mbili mfululizo dakika za 18 na 29.
Kipindi cha pili, Azam FC walitengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao, lakini walifanikiwa kufunga moja tu, Bocco tena daika ya 52.
Kocha Mcameroon Joseph Marious Omog aliwapumzisha  Bocco, Kipre Herman Tchetche na David Mwantika kipindi cha pili na nafasi zao kuchukuliwa na Khamis Mcha ‘Vialli’, Didier Kavumbangu na Said Mourad.
Vialli na Kavumbangu walikwenda kuongeza kasi ya mashambulizi ya Azam FC, lakini safi ya ulinzi KMKm ilisimama imara kukataa kuruhusu mabao zaidi.
Azam FC sasa inafikisha pointi nne baada ya awali kutoa sare ya bila kufungana na wenyeji Rayon katika mchezo wa kwanza, wakati KMKM na timu nyingine zote zina pointi moja kila moja.
Azam FC: Mwadini Ally, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, David Mwantika/Said Mourad (dk 47), Aggrey Moris, Boluo Michael, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sureboy’, Kipre Tchetche/Didier Kavumbangu dk11, Lionel Saint Preux na John Bocco/Khamis Mcha dk65.  
KMKM: Mudathir Khamis, Khamis Ali, Pandu Hajji, Makame Mngwali,  Mwinyi Mngwali, Ibrahim Khatib, Ameir Khamis/Iddi Kambi dk84, Moka Msafiri/Haji Salim (dk 24), Juma Faki, Mudrik Abdullah na Maulid Ramadhan.

Leave a comment