AZAM FC imeanza kwa sare ya bila kufungana na wenyeji Rayon katika mchezo wa ufunguzi Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Kagame Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda.
Azam ilicheza vizuri na bahati haikuwa yao tu hawakuweza kupata mabao na nafasi ambayo wataikumbuka zaidi ni ya mapema tu sekunde ya 24, shuti la Himid Mao ‘Ninja’ lilipogonga mwamba na kwenda nje.
Pamoja na kwamba walicheza nyumbani, lakini Rayon walifurahia sare na mabingwa hao wa Bara, kwani walikuwa kwenye hatari ya kupoteza mchezo.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao/Mudathir Yahya dk89, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’, Kipre Tchetche na Khamis Mcha ‘Vialli’/Didier Kavumbangu dk70.
Rayon Sport; Bikorimana Gerard, Ndayisenga Fuad, Nizigiyimana Karim, Sibomana Bakari, Serugendo Arafat, Tubane James, Leon Uwumbazimana/Hategekimana Aparodis dk67, Sibomana Hussein, Ndatimana Roberts, Yossa Betrand/Sekle Zico dk88 na Motombo Govin/Kambala Salita dk78

Leave a comment