KLABU ya Azam FC ndiyo itakayoiwakilisha Tanzania Bara kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) iliyopangwa kuanza Agosti 8 mwaka huu jijini Kigali, Rwanda.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeiteua Azam kuiwakilisha Tanzania Bara katika michuano hiyo baada ya waandaaji wake, Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuamua kuindoa Yanga iliyokuwa icheze awali.

CECAFA imesema baada ya majadiliano na Yanga kupitia TFF, klabu hiyo ilipewa muda hadi jana (Agosti 4 mwaka huu) iwe imetekeleza matakwa ya kikanuni ili iruhusiwe kushiriki michuano hiyo lakini haikufanya hivyo.
Yanga iliwasilisha orodha ya wachezaji wengi wa kikosi cha pili kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo, jambo ambalo limekatawaliwa na CECAFA kwa vile linakwenda kinyume na kanuni za michuano hiyo.
Azam FC ambayo ilishika nafasi ya pili- nyuma ya Yanga katika ligi iliyopita msimu wa 2012/2013 imekubali kushiriki michuano hiyo na inatarajia kuondoka nchini kesho (Agosti 6 mwaka huu) kwenda Kigali.
Msafara wa Azam FC katika michuano hiyo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, James Mhagama.
Kikosi cha Azam kinatarajiwa kuondoka Alhamisi na kocha Joseph Marius Omog raia wa Cameroon ametuea wachezaji 20.
Hao ni makipa; Aishi Manula, Mwadini Ally, mabeki Waziri Salum, Gadiel Michael, Shomary Kapombe, Abdallah Kheri, Aggrey Morris, Said Mourad na David Mwantika.
Viungo Kipre Balou kutoka Ivory Coast, Salum Abubakar, Mudathir Yahya, Himid Mao, Khamis Mcha ‘Vialli’, Farid Mussa na Joseph Peterson wa Haiti, wakati washambuliaji ni Mrundi Didier Kavumbangu, Leonel Saint- Preux wa Haiti, Kipre Herman Tchetche wa Ivory Coast na John Bocco ‘Adebayor’.