AZAM FC imetoka sare ya 1-1 na Polisi Morogoro iliyopanda Ligi Kuu msimu huu katika mchezo wa kirafiki asubuhi ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mshambuliaji Danny Mrwanda aliyekuwa anacheza Vietnam, alianza kuifungia Polisi Morogoro kabla ya mshambuliaji kutoka Haiti, Leonel Saint-Preux kuisawazishia Azam, mabao yote yakipatikana kipindi cha kwanza.

Polisi inayofundishwa na kiungo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Mohamed ‘Adolph’ Rishard ilicheza soka ya kuvutia dhidi ya Azam FC, ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu. 
Washambuliaji wote wa kigeni wa Azam FC, Ismaila Diara kutoka Mali, Didier Kavumbangu kutoka Burundi, Leonel Saint-Ptreux kutoka Haiti walicheza pamoja na beki Mghana Ben Achaw na viungo Serge Lofo kutoka DRC na Joseph Peterson wa Haiti.
Huo unakuwa mchezo wa kwanza katika mechi za kujiandaa na msimu Azam inashindwa kuondoka na ushindi, baada ya awali kuzifunga 1-0 Ruvu Shooting, 2-1 Friends Rangers, 3-2 kombaini ya Jeshi, 1-0 Polisi Morogoro na 2-1 JKT Ruvu.
Kikosi cha Azam kinakwenda mapumziko ya sikukuu ya Eid El Fitri na kinatarajiwa kurudi mazoezini kuanzia Jumatano wiki ijayo.

Leave a comment