Kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Khamis Mcha 'Vialliakishangilia bao lake la pili aliloifungia Tanzania, Taifa Stars katika sare ya 2-2 na Msumbiji Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco. Vialli alitokea benchi na kuifungia mabao yote mawili Stars dhidi ya Mambas.