MSHAMBULIAJI mpya wa Azam FC kutoka Mali, Ismaila Diara amesema kwamba atajihitaji muda kuzoea mazingira ya soka ya Tanzania kabla ya kuanza kuwika.
Akizungumza wiki hii Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam mchezaji huyo mwenye mwili mkubwa amesema kwamba hajui lolote kuhusu soka ya Tanzania na yote atajifunza hapa
“Sijui, sijui kabisa, mimi ni mchezaji na naweza kucheza popote. Nitahitaji muda kidogo nizoee, ila nina amini nitafanya vizuri,”amesema.

Leave a comment