Kocha Mkuu wa Azam FC, Mcameroon Joseph Marius Omog akiwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JKN), Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuanza kuiandaa timu yake kwa mashindano ya msimu ujao. Azam wataanza kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Agosti mwaka huu wakati mapema mwakani watashiriki Ligi Mbingwa Afrika.