MABINGWA wapya wa Ligi Kuu ya Voidacon Tanzania Bara, Azam FC usiku wa jana walitamba katika sherehe za tuzo za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenye ukumbi wa Golden Jubilee, Tower, Mtaa wa Ohio, Dar es Salaam.
Mshambuliaji wake kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi hiyo msimu wa 2013-2014 akiwapiku Anthony Matogolo wa Mbeya City na Lugano Mwangama wa Prisons.
Kwa ushindi huo, Kipre alizawadiwa kitita cha Sh. Milioni 5.2 wakati kipa wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Hussein Sharrif ‘Cassilas’ ameshinda tuzo ya mlinda mlango bora wa Ligi Kuu akiwapiku David Burhan wa Mbeya City na
Juma Mwambusi Mwambusi wa Mbeya City, alishinda tuzo kocha bora, akiwaangusha Charles Boniface Mkwasa wa Yanga SC na Mecky Mexime wa Mtibwa Sugar na kupewa Sh. Milioni 5.2. 
Refa Israel Mujuni Nkongo wa Dar es Salaam ameibuka mwamuzi bora akilamba Sh. milioni 7.8 baada ya kuwabwaga Isihaka Shirikisho wa Tanga na Jonasia Rukia wa Kagera walioingia kwenye kipengele hicho.  
Tuzo ya Mfungaji bora wa msimu ilikwenda kwa mshambuliaji wa Simba, Mrundi Amisi Tambwe.
Tambwe aliyefunga magoli 19, alizawadiwa Sh. milioni 5.2.
Tambwe aliwashinda Elias Maguri wa Ruvu Shooting, Kipre Tchetce wa Azam FC wote mabao 13, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza wote wa Yanga SC ambao wote walifunga mabao 12 kila mmoja
Yanga SC imeibuka timu yenye nidhamu kwa mara nyingine baada ya kutwaa tuzo hiyo pia msimu wa 2012/13 wa Ligi Kuu na kuzawadiwa Sh. Milioni 16 ikizipiku Azam FC na JKT Oljoro.
Zawadi nyingine zilizotolewa ni pamoja na Sh. milioni 75 iliyokwenda kwa Azam FC waliotwaa ubingwa, Yanga SC Sh. milioni 35, Mbeya City Sh. milioni 26 na Simba SC Sh. 21.
Hakukuwa na mchezaji hata mmoja kati ya walioshinda tuzo zao kutokana na wachezaji hao kuwa mapumzikoni baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu na wote walipokelewa tuzo zao.
Juma Mwambusi yuko Sudan na timu yake wakishirki michuano ya Nile Basin, naye alipokelewa tuzo yake na Katibu Mkuu wake, Emmanuel Kimbe.

Leave a comment