Kevin Friday wa Azam FC akimtoka beki wa Kenya wakati akiichezea Ngorongoro
 

Kevin Friday wa Azam FC akimtoka beki wa Kenya wakati akiichezea Ngorongoro
 
TIMU ya soka ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imeitoa Kenya katika Raundi ya Kwanza ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Senegal kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya jumla ya bila kufungana nyumbani na ugenini.
Kwa matokeo hayo, Ngorongoro inayofundishwa na kocha mzalendo John Simkoko sasa itamenyana na Nigeria katika hatua inayofuata.
Penalti za Tanzania zilikwamishwa nyavuni na Mohammed Hussein, Kevin Friday, Mange Chagula na Iddi Suleiman, wakati Mudathir Yahya alikosa.
Penalti za Kenya zilifungwa na Geoffrey Shiveka, Timonah Wanyonyi na Victor Ndinya, wakati Evans Makari na Harison Nzivo walipoteza.
Hakuna kipa aliyeokoa penalti bali wapigaji waliokosa walipiga nje.
Ilikuwa mechi kali na ya ushindani na makipa wa timu zote mbili, Aishi Manula wa Tanzania na Farouk Shikhalo wa Kenya aliyeanza kabla ya kumpisha Boniface Barasa dakika ya 88 walifanya kazi nzuri ya kuokoa michomo ya hatari

Leave a comment