Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akimfariji beki wa Azam FC,Samih Haji Nuhu kabla ya mchezo wa jana wa kirafiki wa kimataifa kati ya Tanzania na Burundi ambao walishinda 3-0. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Burundi (FFB) Reverien Ndikuriyo. Beki huyo wa Azam FC amerejea hivi karibuni kutoka nchini Afrika Kusini kufanyiwa upasuaji wa goti hilo.