WACHEZAJI wa Azam FC wamepewa likizo hadi Juni 15, mwaka huu baada ya kumaliza msimu vizuri wakitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Wachezaji na viongozi wa Azam FC jana walikuwa na kikao maalum na bodi kwa ajili ya kupongezana na kuagana kwa likizo hiyo ndefu, wakajipange kwa ajili ya msimu ujao.
Katibu wa klabu, Nassor Idrissa Mohamed ‘Father’ amesema benchi la Ufundi kwa pamoja na wachezaji wanakwenda likizo vizuri baada ya mafanikio ya msimu huu.
Azam imemaliza Ligi Kuu na pointi 62 dhidi ya 56 za waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga SC na kuwa timu ya kwanza nje ya Simba na Yanga kutwaa ubingwa wa Bara tangu mwaka 2000 Mtibwa Sugar ilipofanya hivyo.
Azam inakuwa timu ya saba nje ya Simba SC kutwaa taji la Ligi Kuu, baada ya Cosmo mwaka 1967, Mseto mwaka 1975, Pan Africans mwaka 1982, Tukuyu Stars mwaka 1986, Coastal Union 1988 na Mtibwa Sugar mara mbili mfululizo 1999 na 2000.
Wakati huo huo: Wachezaji wa akademi ya Azam nao pia wamepewa likizo hadi Mei 8, mwaka huu watakaporejea kuenedelea na mafunzo ya soka ya kisasa.

Leave a comment