KOCHA Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga amewachukua makipa wote wa mabingwa wapya wa Bara, Azam FC Mwadini Ally na Aishi Manula katika kikosi chake cha wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini kesho (Aprili 20 mwaka huu) kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu.
Kwa ujumla, Mayanga amechukua wachezaji saba wa Azam FC wengine ni mabeki Aggrey Morris, Erasto Nyoni na Said Moradi na viungo Himid Mao na Khamis Mcha
Kikosi kamili cha Stars ni makipa; Aishi Manula (Azam FC), Mwadini Ally (Azam FC) na Deogratias Munishi (Yanga SC). 
Mabeki Abdi Banda (Coastal Union), Aidan Michael (Ruvu Shooting), Aggrey Morris (Azam FC), Erasto Nyoni (Azam FC), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kelvin Yondani na Said Moradi (Azam FC).
Viungo; Amri Kiemba (Simba SC), Frank Domayo (Yanga SC), Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC). 
Washambuliaji; Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba SC), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam FC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga SC), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba SC), Simon Msuva (Yanga SC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).
Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).
Washambuliaji ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga Athanas Fabian (Mbeya). Taifa Stars  itaingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.

Leave a comment