BAO la dakika ya 75 la kiungo mtaalamu wa Azam Veterans, Nassor Idrissa Mohammed ‘Father’ jioni hii limeinusuru timu hiyo kuzama mbele ya Wazee Veterans ya Zanzibar baada ya kupata sare ya 3-3 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Nassor alifunga bao hilo kwa ufundi wa hali ya juu baada ya kazi nzuri ya Vivek Nagul aliyekuwa akicheza pamoja naye katika safu ya kiungo hii leo.

Azam ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Abdulkarim Amin ‘Popat’ dakika ya saba na Kally Ongalla dakika ya 30, lakini kipindi cha pili Wazee inayoundwa na wachezaji wa zamani wa kimataifa wa Zanzibar ilifanikiwa kusawazisha ndani ya 13 za kipindi cha pili.
Alianza Abdallah Matake Kassim dakika ya 49 na baadaye Mbaraka Nyangi dakika ya 57 ambaye pia alifunga bao la tatu dakika ya 64, kabla ya Father kuiepusha na aibu ya kufungwa nyumbani Azam Veterans.
Bao tamu kuliko yote hii leo ni lile lililofungwa na Kali Ongala aliyefumua shuti kutoka katikati ya Uwanja.