Mshambuliaji wa Azam Academy, Sadallah Mohamed akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Turkey FC ya Ligi Daraja la Pili Zanzibar katika mchezo wa kirafiki uliofanyika asubuhi ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Tusker FC ilishinda 2-1 mabao yake yakifungwa na Khalid Hamad na Ridha Hamis, wakati bao la Azam lilifungwa na Mgaya Abdul.