KIKOSI cha Azam FC, kinaondoka asubuhi ya leo Dar es Salaam kwa ndege kwenda Mbeya kwa ajili ya pambano la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Mbeya City Council (MCC) Jumapili Uwanja wa Sokoine mjini humo.
Azam inakwenda huko ikihitaji ushindi ili kuongeza matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara- hivi sasa rasmi ikiwa inahitaji pointi tatu zaidi kujihahakishia kuwavua taji hilo, Yanga SC.

Kocha Mcameroon wa Azam FC, Joseph Marius Omog alikuwa mwenye furaha baada ya ushindi wa 3-0 juzi Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani dhidi ya wenyeji Ruvu Shooting, lakini akasema shughuli haijaisha. “Ni furaha. Ni ushindi mzuri, tumevuka kikwazo kimoja, vijana waliuanza mchezo vizuri wakizingatia nilichowaambia. Karibu kila mmoja alitekeleza majukumu yake vizuri. Wapinzani walikuwa wagumu, lakini tumechukua pointi tatu,”alisema.
Omog alisema anajivunia wachezaji wake na hana cha kuwaambia zaidi ya asante pamoja kama timu na akawataka kuendeleza mshikamano huo daima. Hata hivyo, Omog amewaambia wachezaji wake kwamba wanahitaji kushinda pia mechi mbili za mwisho ili wamalize ligi vizuri.
Ushindi huo umeifanya Azam FC ifikishe pointi 56 baada ya kucheza mechi 24 na kujivuta karibu kabisa na chumba kinachohifadhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu, ikiwaacha kwa pointi nne mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 52 za mechi 24 pia.
Timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake, baada ya mechi ya kesho itacheza mechi ya mwisho dhidi ya JKT Ruvu Aprili 19, Uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.