MECHI kati ya wenyeji Ruvu Shooting na Azam FC ya Dar es Salaam iliyokuwa ifanyike jioni ya leo Uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani imeahirishwa hadi kesho kufuatia mvua kubwa.
Timu hazikuwahi hata kuingia uwanjani kupasha misuli moto kutokana na mvua kubwa na Uwanja kujaa maji na ilipowadia Saa 10:20 waamuzi wa mechi hiyo waliingia uwanjani kukagua na kuvunja mchezo.
Kilifuatia kikao cha pande zote nne, baina ya viongozi wa Ruvu na Azam pamoja na TFF na marefa ambao waliafikiana mechi ichezwe kesho iwapo hali itakuwa nzuri.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ alikuwepo na kushuhudia hali hiyo.
Isihaka Shirikisiho wa Tanga ndiye aliyetarajiwa kuwa refa wa mchezo wa leo, akisaidiwa na Hassan Zani na Agness Pantaleo wote wa Arusha na refa wa akiba mwenyeji, Simon Mbelwa.
Azam yenye pointi 53 inaendelea kuishi kileleni mwa Ligi licha ya Yanga SC kuifunga Kagera Sugar 2-1 mjini Dar es Salaam, kwani wana Jangwani hao wanatimiza pointi 52 huku pia wakiwa wamecheza mechi moja zaidi