Kutoka kushoto Makiada Franco, Bryson Raphael na Aishi Salum

AZAM FC itamkosa mchezaji wake chipukizi anayeinukia vizuri, Bryson Raphael katika mchezo wake wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Meneja wa Azam FC, Jemadari Said amesema mchezaji huyo amerejea kutoka Kenya alipokwenda kuichezea timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes akiwa anachechemea kwa maumivu ya kifundo cha mguu.

Jemadari amesema hilo ni pigo kwa timu kwa sababu huyo ni miongoni mwa wachezaji muhimu, lakini kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog atalazimika kumuondoa mchezaji huyo katika programu yake ya kesho.
Tayari Azam FC inawakosa Samih Haji Nuhu, Joseph Kimwaga, Ismail Gambo ‘Kussi Jr’, Farid Mussa na Ibrahim Mwaipopo ambao wote ni majeruhi kwa muda mrefu sasa.