MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Joseph Kimwaga Lubasha ameanza mazoezi mepesi baada ya kupata ahueni ya maumivu ya goti yaliyokuwa yakimsumbua.
Kimwaga amepewa programu maalum na dawati la tiba la Azam FC, chini ya Daktari Mkuu, Mwanandi Mwankemwa ambayo anaendelea hivi sasa.
Mchezaji huyo anatarajiwa kurejea rasmi uwanjani msimu ujao, baada ya kuwa nje kwa miezi miwili ya mwisho ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.

Umaarufu wa Kimwaga aliyepandishwa kutoka timu ya vijana msimu huu, ulikuja baada ya kuifungia Azam FC bao la ushindi wa 3-2 dhidi ya Yanga SC Septemba 22, mwaka jana.
Mbali na Kimwaga, wachezaji wengine majeruhi Azam FC ni beki wa kati, Ismail Gambo ‘Kussi Jr’ ambaye ataendelea kuwa nje kwa miezi miwili zaidi, viungo Farid Mussa na Ibrahim Mwaipopo ambao wote watakuwa nje kwa zaidi ya mwezi mmoja, maana yake kwa msimu huu hawatacheza tena.